Nyumbani
Pilato wa Yanga, Mamelod huyu hapa
MWAMUZI Dahane Beida kutoka Mauritania ndiye atakuwa pilato wa mchezo wa marudiano kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns.
Yanga inaingia katika mchezo huo ikihitaji ushindi au sare yoyote ya mabao ili kutinga hatua ya nusu fainali baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuisha kwa suluhu.
Mwamuzi huyo pia anakumbukwa kwani alichezesha mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita wakati Yanga iliposhinda bao 1-0 dhidi ya USM Alger katika mechi ya marudiano iliyopigwa jijini Algeria Juni 3, mwaka jana.