Nyumbani

Master Rim FC yawaza Ligi Kuu

KOCHA wa klabu ya Master Rim FC, Ally Haji amesema ili kufikia malengo ya kucheza Ligi Kuu Bara uongozi unapaswa kuongeza wachezaji wenye viwango bora na kuongeza nguvu benchi la ufundi.

Awali akizungumzia mipango, mmiliki wa timu hiyo, Kassim Ahmed amesema kwasasa wanakamilisha usajili kushiriki Ligi Daraja la Tatu na baada ya hapo wamejiandaa kwa kuzingatia kuwa ⁠bajeti yao inatosha kucheza mashindano makubwa.

Akizungumza na HabariLEO, Haji amesema timu iliyopo kwa sasa ni nzuri inayowezesha kushindana katika ngazi za chini ila kuna haja ya kuongeza nguvu kufikia malengo.

“Kiufundi itafanikisha malengo na tutaongeza wachezaji ili malengo yetu yatimie na kwa benchi la ufund lazima liongezeke,” amesema.

Master Rim FC ni timu ambayo kwa sasa inakamilisha hatua za mwisho za usajili kushiriki ligi daraja la tatu za mikoa, iliwahi pia kucheza mashindano ya Ndondo Cup msimu uliopita pamoja na mashindano ya Ramadhan Cup.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button