Mutima Wangu awapa somo ma-Ex: “Ukiona hapokei, usipige tena”

DAR ES SALAAM:MSANII wa Bongo Fleva kutoka Kings Music, Mutima Wangu, ambaye yupo chini ya lebo ya Ali Kiba ‘King Kiba’, ametoa ujumbe kwa watu ambao wanapata ugumu wa kuendelea na maisha baada ya kuachana na wapenzi wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mutima Wangu amewashauri watu wenye tabia ya kuendelea kuwasiliana na wapenzi wao wa zamani, hasa pale ambapo ex huyo tayari ameendelea na maisha na kuwa kwenye mahusiano mengine.
Msanii huyo amesema mtu akiona ex wake hapokei simu, anapaswa kujiongeza na kuacha kuendelea kumpigia mara kwa mara kwa matumaini ya kurudiana.
Katika ujumbe wake, Mutima Wangu ameandika:
“Kama wewe ni mtu wa kupenda kula vitu vilivyobaki, tafadhali badilika! Maana tabia hiyo ikizidi, siku moja utajikuta unamrudia hata ex wako ukisema, ‘Huyu bado hajaharibika.’
Hivi ex wako akikupigia simu saa nane za usiku, anadhani bado uko single au bado hajajua umeendelea na maisha? Ujumbe kwa ma-ex: hana mazoea sasa.
Kama umemmiss, utajua mwenyewe cha kufanya. Usipige simu mara kwa mara kwa mtu ambaye tayari ana mtu wake. Huyo mtu si single tena bana, Ukiona hapokei, usipige tena… labda yupo busy kukusaidia usimsahau kabisa.”
Ujumbe huo umejikita katika kuwakumbusha watu kuheshimu mipaka ya wapenzi wao wa zamani na kukubali pale ambapo kila mmoja ameendelea na maisha yake.




