Nyumbani

Ndimbo: Mambo yanakwenda vizuri Taifa Stars

DAR ES SALAAM: TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeendelea na maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Guinea-Bissau, huku wachezaji wanaocheza nje ya nchi wakiendelea kuwasili kujiunga na kikosi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amesema baadhi ya wachezaji tayari wamewasili na kuripoti kambini, huku wengine wakitarajiwa kuwasili kabla ya mchezo huo.

Ndimbo amewataja baadhi ya wachezaji waliowasili kuwa ni Alphonce Mabula, Simon Msuva, Cyprian Kachewele na Kibu Dennis.

Amesema wachezaji wengine watawasili leo na wengine kesho, kutokana na majukumu yao binafsi na taratibu za safari kutoka maeneo mbalimbali.

Aidha, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia Taifa Stars katika mchezo huo muhimu.

Mchezo huo dhidi ya Guinea-Bissau unatarajiwa kuchezwa Septemba 25, kwenye Uwanja wa Amani, Zanzibar.

 

Related Articles

Back to top button