Afrika Mashariki

FKF yaweza kuvuna mabilioni kupitia mpango mpya wa FIFA

SHIRIKISHO la Soka Kenya (FKF) linaweza kujipatia mabilioni ya fedha endapo wanachama wa FIFA wataidhinisha mpango mpya wenye utata wa kuuza sehemu ya hisa za biashara zinazohusisha kombe la Dunia.

Mpango huo unahusisha kuundwa kwa kampuni mpya iitwayo FIFA Forward Enterprise (FFE), ambayo itasimamia shughuli za kibiashara za FIFA kama haki za matangazo, udhamini, tiketi na leseni, huku wawekezaji wakiruhusiwa kununua hisa ndogo zisizo na mamlaka ya kufanya maamuzi.

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, FIFA inalenga kuongeza zaidi ya dola bilioni 10 kwa ajili ya maendeleo ya soka duniani. Kila shirikisho mwanachama, likiwemo FKF, linaweza kunufaika kwa kupokea takribani dola milioni 20 (zaidi ya Sh bilioni 50 za Tanzania), fedha ambazo linaweza kuziwekeza au hata kuuza hisa zake kulingana na masharti yatakayowekwa.

Hata hivyo, mpango huo umekumbana na upinzani mkali kutoka UEFA, ambayo imeonya kuwa kuuza hisa za mashindano makubwa kama Kombe la Dunia kunaweza kuhatarisha uwazi na misingi ya uendeshaji wa soka duniani.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ametetea mpango huo akisema utasaidia kuongeza fedha za kuendeleza soka katika nchi zote wanachama huku FIFA ikiendelea kubaki na mamlaka kamili ya kusimamia mashindano na maamuzi ya kiutawala

Related Articles

Back to top button