
MICHEZO mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara inapigwa leo Dar es Salaam na Mwanza.
JKT Tanzania inayoshika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 26 baada ya michezo 24 itakuwa uwanja wa nyumbani wa Mej Gen Isamuhyo, Mbweni kuikaribisha Geita Gold iliyopo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 24.
Kwenye uwanja wa CCM Liti mjini Singida, Dodoma jiji iliyopo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 28 baada ya michezo 23 itakuwa mgeni wa Singida Big Stars inayoshika nafasi 11 ikiwa na pointi 26 baada ya michezo 24.
KMC inayoshika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 32 baada ya michezo 24 itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar iliyopo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 29 kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.