Fadlu hana presha na Waangola
DAR ES SALAAM: KUELEKEA mchezo wa Kesho wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos do Maquis, Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema amewaandaa wachezaji wake kwa mbinu bora kuweza kufanya vizuri.
Amesema wameshafanya maandalizi ya kutosha ili kupata alama tatu dhidi ya Bravos katika mchezo utakaochezwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
“Licha ya kufanikiwa kuona ubora wa Bravos lakini mchezo wa Pamba Jiji FC umutusaidia kuimarisha kuboresha kikosi chetu kuelekea mchezo wa kesho,” amesema.
Fadlu amesema hana presha na aina ya mchezo huo licha ya kuwa kikosi chake kimejaa vijana wengi ambao ni wageni katika mashindano hayo ya Afrika ukiachana na wachezaji wachache kama Che Malone Fondoh.
Kwa upande wake, Che Malone Fondoh amesema wachezaji wote wapo tayari kusikiliza mipango ya kocha wao na kupata ushindi mnono katika ardhi ya nyumbani.