
KOCHA wa Ihefu, Juma Mwambusi amesema pamoja na timu yake kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi kuu lakini inaimarika.
Akizungumza na Spotileo kocha huyo amesema hiyo ni ishara njema kwamba muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa kimekaa sawa na kuanza kufurahia ushindi.
“Najua uongozi wa timu na mashabiki wanaumizwa na matokeo haya lakini siku si nyingi yatapotea sababu tayari timu imeanza kujenga muunganiko ndio manaa tunacheza soka la kuvutia na mapungufu kidogo ndiyo yanatugharimu,” amesema Mwambusi.
Ihefu inashika nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 9. Imeshinda mchezo 1, kupoteza 6 na sare 2.
Mchezo wa Ligi Kuu unaofuata wa Ihefu utakuwa Novemba 12 dhidi ya Simba.