‘Kim Kardashian’matatani

MAREKANI: Mwanamitindo na mfanyabiashara kutokea nchini Marekani, Kimberly Noel ‘Kim Kardashian’ anakabiliwa na kesi baada ya kosa alilofanya kwenye chapisho lake la Instagram mwezi Februari 2024.
Kupitia InstaStory msanii huyo alikuwa akihimiza watu kusaini ombi la kusitisha adhabu ya kifo kwa Ivan Cantu, ambaye alidaiwa kuwa alikuwa gerezani Texas kwa hukumu ya kifo.
Hata hivyo, alitumia picha ya mtu mwingine aitwaye Ivan Cantu, ambaye ni meneja wa mradi mjini New York.
Ivan Cantu wa New York sasa amemfungulia Kim Kardashian kesi, akidai kuwa alikumbana na fedheha na kudhalilika hadharani kutokana na chapisho hilo.
Hii ilitokea muda mfupi kabla ya Ivan Cantu aliyekuwa gerezani Texas kuuawa kwa hukumu ya kifo, licha ya madai ya kutendewa haki.