Serie A

Conte atoa neno kuhusu Osimhen

ITALIA: MENEJA wa Napoli, Antonio Conte, anasema mchezaji wake Victor Osimhen lazima aendelee kufanya kazi kwa bidii licha ya mustakabali wake kutokuwa na uhakika wa kubaki katika klabu hiyo.

Osimhen alikuwa na makubaliano na Napoli kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto.

Licha ya Chelsea kuonyesha kumuhitaji mchezaji huyo lakini kwa sasa hakuna klabu yeyote barani Ulaya iliyo tayari kulipa euro milioni 130 katika mkataba wa mchezaji huyo.

Conte alisema hana uhakika Mnigeria huyo atacheza wapi msimu ujao.

“Nilizungumza na Victor na hakuna mabadiliko katika hali yake. Yeye ni mchezaji bora,” Conte alisema katika nukuu iliyotolewa na mtaalamu wa masuala ya uhamisho ya wachezaji, Fabrizio Romano.

“Yeye ni mchezaji wa Napoli kwa hivyo anahitaji kufanya kazi kwa bidii, hata kama kuna uwezekano wa kuondoka ila bado hatujui mwisho wa sakata lake la uhamisho.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button