Habari Mpya

Bentancur atazikosa Arsenal, Everton na Hoffenheim

LONDON: KIUNGO wa Tottenham Hotspur Rodrigo Bentancur atakuwa nje kwa wiki mbili kufuatia jeraha la kichwa katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa kombe la Carabao dhidhi ya Liverpool Jumatano wiki hii katika uwanja wao wa nyumbani

Taarifa zinaeleza kuwa Bentancur alianguka vibaya akijaribu kupiga kichwa mpira wa kona wa Pedro Porro wakati Spurs walipokuwa wakilishambulia lango la Liverpool mapema kipindi cha kwanza.

Akizungumza na wanahabari kocha wake Ange Postecoglou amethibitisha kukosekana kwake akisema kiungo huyo kwa sasa anaendelea vizuri baada ya timu ya madaktari kuhangaika kumuweka sawa

“Jambo zuri kwa sasa ni ameruhusiwa kurudi nyumbani na anaendelea vyema, lazima tufuate itifaki, tumuangalie kwa wiki kadhaa kisa tuone itakuwaje” amesema Postecoglou

Ukiacha mchezo wa FA dhidi ya Tamworth, Bentancur pia ataukosa mchezo wa dabi dhidi ya Arsenal kwenye ligi kuu wiki ijayo, mchezo dhidi ya Everton na ule wa Europa league dhidi ya Hoffenheim Januari 23

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button