Nyumbani

Benchikha ataka viwango Simba

KOCHA Mkuu mpya wa Simba, Abdelhak Benchikha ametambulishwa rasmi katika klabu hiyo akisema hataangalia majina bali kiwango cha mchezaji.

Akizungumza Dar es Salaam leo Benchikha amesema jambo kubwa analoomba ni mashabiki kushirikiana na benchi la ufundi na anaamini kupitia hilo klabu itafanikiwa kwa pamoja.

“Mafanikio yatajengwa na wanasimba wote hilo ndio muhimu zaidi. Kwa wachezaji sitaangalia majina bali anayefanya vizuri, kiwango cha mchezaji ndio kitafanya nimtumie,” amesema Benchikha.

Benchikha amechukua nafasi ya kocha Roberto Oliveira Goncalves De Carmo(Robetinho) alipewa ‘Thank You’ Novemba 7, 2023.

Related Articles

Back to top button