Nyumbani

Yanga yaoga ‘minoti’

DAR ES SALAAM. UONGOZI wa Yanga umeridhia ombi mdhamini wao Sportpesa kuhitaji makombe waliyopata msimu wa 2023\2024 kupelekwa kwenye ofisi hizo ikiwa sehemu ya kutambua mchango wao katika miaka saba ya udhamini wao.

Kauli hiyo imetolewa leo baada ya Yanga kukabidhiwa na Sportpesa mfano wa hundi yenye thamani ya million 537.5 ikiwa ni sehemu ya ‘bonus’ ya mafanikiwa ya msimu wa 2023\24 ulitamatika hivi karibuni.

Hundi hiyo wamekabidhiwa leo na wadhamini wao Sportpesa baada ya kufanikisha malengo yao ikiwemo kutetea mataji ya mawili kwa msimu huu ikiwemo Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la CRDB Bank baada ya kumfunga Azam FC kwa penalti ya 5-6, mchezo uliochezwa uwanja wa New Amaan, Visiwani Zanzibar.

Akizungumza na spotileo, Rais wa Yanga, Hersi Said amesema wamepokea na kufanyia kazi maombi hayo ya mdhamini huyo mkuu kuhakikisha wanapeleka makombe hayo siku ya jumatatu ijayo.

Amesema wanajivunia kushirikiana na Sportpesa, wanaendelea kutengeneza mahusiano mazuri na kampuni hiyo na kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwa namba mmoja Tanzania.

“Nichukue nafasi hii kuishukuru sportPesa kwa kutekeleza Kwa wakati makubaliano yaliyopo kwenye mkataba kwa kutoa ‘bonus’ baada ya klabu yetu kutwaa ubingwa huu Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho, tumefurahi sana kupokea rasmi zawadi hii ya ‘bonus’, kimkataba kwa kushinda Ligi Kuu, Shirikisho na kufikia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Hersi.

Anawaahidi wataendelea kuijenga timu imara na ushindani mkubwa ndani na nje ya Tanzania ikiwemo kufikia malengo ya kutaka kucheza nusu fainali ya Afrika kwa msimu ujao ambapo itasaidia kumtangaza mdhamini huyo.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Tarimba Abass, alisema ‘bonus’ hiyo ni baada ya klabu hiyo katika ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na robo fainali CAF msimu wa 2023/24.

“Sportpesa imekuwa imejivunia mahusiano ya kiudhamini kati ya kampuni na Yanga, hapajawahi kitokea muda wa kujutia kwa sababu ya uendeshaji wao wa kiweledi na tumefikia malengo yetu, tulichokiahidi tumekitekeleza bila kuchelewa, kiasi cha milioni 537.5,” amesema Tarimba.

Related Articles

Back to top button