Bacca:Nataka kuwa mfungaji bora

DAR ES SALAAM:BEKI wa Yanga, Ibrahim Bacca ameamua kufuata nyayo za aliyekuwa beki wa Barcelona, Ronald Koeman aliyewahi kufunga jumla ya mabao 250 katika kipindi chake akiwa mwanasoka.
“Msimu huu nimeweka nia ya kutaka kufunga katika kila mechi, nahitaji kunyakuwa tuzo ya ufungaji bora,na nina imani nitafikia malengo yangu,” amesema Beki huyo.
Malengo ya Bacca kufunga idadi ya mabao mengi kwa msimu huu ni kutaka kuweka historia yake lakini sio jambo jipya kwa mabeki, iliwahi kufanywa na baadhi ya wachezaji wa kimataifa na miongoni mwao ni Koeman.
Mholanzi huyo aliyezaliwa Machi 21, 1963 ndiye Kocha Mkuu wa timu ya taifa Uholanzi kwa sasa. Aliwahi kucheza Barcelona, Ajax, PSV, Feyenoord lakini pia, aliwahi kuzifundisha klabu hizo na nyingine.
Koeman alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi ya beki na kama kiungo, kwa sababu ya upachikaji wake wa mabao, anachukuliwa kuwa mmoja wa walinzi bora wa kati wa muda wote.