Yanga raha, Simba, Azam kivumbi
WAKATI bingwa mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ikipokea kombe leo, Azam na Simba zitashuka viwanja tofauti kusaka pointi muhimu zikigombea kushika nafasi ya pili.
Yanga itakuwa mwenyeji wa Tabora United kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam mchezo utakaotumika kukabidhiwa taji hilo walilolitwaa msimu wa 2023/2024.
Simba inayoshika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi na ikisaka ushindi kwa udi na uvumba ikiwa na pointi 63 sawa na Azam itakuwa wenyeji wa KMC kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Nayo Azam iliyopo nafasi ya 2 inayotaka kusalia kwenye nafasi hiyo hadi mwisho wa ligi itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Michezo mingine ya raundi ya 29 itakayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
Coastal Union vs JKT Tanzania
Ihefu vs Dodoma Jiji
Mashujaa vs Mtibwa Sugar
Namungo vs Tanzania Prisons
Singida Big Stars vs Geita Gold