Ligi Kuu

Azam bado haijamaliza, yampiga pini Mubiru

DAR ES SALAAM: BAADA ya kuanzisha moto kwenye dirisha la usajili, Azam FC bado haijaonesha dalili za kushusha kasi. Matajiri hao wa Chamazi wamemtambulisha winga wa kimataifa wa Uganda, Mubiru Hassan, huku wakitarajia kutangaza nyota mwingine leo jioni katika harakati za kukijenga kikosi cha ushindani kwa msimu mpya.

Mubiru ametua Azam akitokea Sports Club Villa ya Uganda, ambako alijizolea sifa kutokana na uwezo wake wa kucheza pembeni na kutengeneza nafasi za mabao.

Usajili wa Mubiru unaongeza idadi ya nyota wapya waliowasili Chamazi baada ya klabu hiyo hivi karibuni kuwatambulisha winga Enock Molia aliyekuwa akiichezea St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mabeki wa kati Lupini Dieumerci kutoka AS Maniema Union na Henri Stanic na kumrejesha Kipre Junior.

Kwa mujibu wa taarifa ya Azam, haijaweka mwisho wa usajili wake, huku ikitarajia kutangaza mchezaji mwingine leo jioni katika mwendelezo wa kuimarisha kikosi chake.

Azam imeweka nguvu kubwa katika dirisha hili la usajili ikiwa na lengo la kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako itaiwakilisha Tanzania msimu huu.

Kwa usajili unaoendelea kufanywa, ni wazi Azam imekusudia kuongeza ushindani katika kikosi chake na kumpa Kocha Florent Ibenge chaguo pana kuelekea msimu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button