AFCON

Ame aipa nafasi Stars AFCON 2025

DAR ES SALAAM: BAADA ya Droo ya Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, Beki wa Mashujaa FC na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Ibrahim Ame amesema anaamini Tanzania itafanya vizuri na kuvuka kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Droo ya AFCON imeshirikisha timu 24 zilizofuzu, Tanzania imepangwa kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda kwa ajili ya fainali hizo zinazotarajiwa kufanyika Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026
Ibrahim, amesema kundi ni gumu na kunatakiwa  kufanyika maamdalizi ya mapema kijiandaa na fainali hizo kwa ajili ya kufikia malengo.

“Tukianza maandalizi mapema, ninaimani tunaweza kufanya vizuri hakuna timu rahisi katika kundi letu, tukiweza kumfunga Nigeria na Uganda matarajio yetu yatatimia. Uganda itakuwa ni mechi ngumu sana kwa sababu tunafahamiana vizuri, pia tutambue kuwa kuna wachezaji wao wanacheza ligi ya Tanzania na tunafahamiana vizuri,” amesema.

Amesema hana presha na benchi la ufundi la Stars pamoja na wachezaji wenzake kwa sababu malengo ni kuvuka makundi hayo na kusonga mbele na kutorudia makosa ya kuondolewa mapema katika fainali hizo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button