Ligi Kuu

Chama ameaga bwana

Ni takribani kilomita 0.6 ametumia Clatous Chama kutoka Makao Makuu ya Klabu ya Simba SC, Msimbazi kwenda ‘Twiga Street’ Jangwani na hatimaye ‘Magician’ huyo ameaga rasmi.

Chama anayeufanya mchezo wa soka kuonekana kama kula ice cream ya maziwa au kunywa asali huku ukiwa na smartphone ukitizama picha za Hamisa Mobeto, ametumia miaka sita kuifikisha Simba robo fainali mara nne akiwa Msimbazi.

Yanga walimtambulisha Chama siku tatu zilizopita, hata hivyo barua ya Chama imejibu sintohamu za kwanini alishindwa kutokea kwenye hafla za kula keki, na kushindwa kubadili utambulisho wake Instagram.

“Baada ya miaka sita ya furaha, majivuno na malengo, hatima zetu zilizounganishwa zinachukuwa mkondo mwingine, sina cha kuwalipa zaidi ya heshima kwa kila mmoja wenu kwa mapenzi na kuniunga mkono kwa miaka yote na hakuna atakayebadili historia tuliyotengeneza pamoja,” ameandika Chama kwenye Instagram yake.

Sasa fundi huyo wa soka atawatumikia Wananchi msimu ujao. Itoshe kusema Wanasimba wanapaswa kukubaliana na ukweli kuwa kipenzi chao kimetoeka mitaa ya Msimbazi Kariakoo.

Related Articles

Back to top button