EPLKwingineko

Ni wiki ya pata potea EPL

KLABU ya Arsenal ina nafasi ya kuongoza kwa alama nane katika msimamo wa Ligi Kuu England(EPL) itakapoivaa Crystal Palace mwisho wa wiki hii.

Ushiriki wa Manchester City katika Kombe la FA na kisha mapumziko ya michezo ya kimataifa ina maana kikosi cha Pep Guardiola hakitacheza mchezo wa ligi hadi Aprili Mosi kitakapoikaribisha Liverpool uwanja wa Etihad.

Baadhi ya wachezaji wa Manchester City katika moja ya michezo ya timu hiyo.

City ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Liverpool Oktoba 16, 2022 na iwapo itapoteza tena, Arsenal inaweza kuongoza kwa alama nyingi zaidi iwapo itaifunga Leeds United inayosuasua.

Timu hizo za juu katika msimamo wa EPL zina michezo ijayo inayofanana mwisho wa msimu, kila moja ikizikabili timu zinazopambana kujiokoa kushuka daraja pamoja na timu zinazogombea nafasi kucheza Kombe la Europa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button