Kwingineko

Mashabiki 59 wa PSG wakamatwa Ujerumani

STUTTGART: Polisi mjini Stuttgart nchini Ujerumani wamesema wanawashikilia mashabiki 59 wa vigogo wa soka la Ufaransa PSG kuepusha vurugu zinazoweza kutokea kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya leo usiku dhidi ya wenyeji wa dimba la MHP Arena Vfb Stuttgart.

Klabu hiyo ya Ujerumani itawakaribisha PSG katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo timu zote zikigombea nafasi ya kucheza playoff ambayo itawapeleka hatua ya 16 bora.

Polisi wamesema wamepata taarifa za kiitelijensia za uwepo wa vurugu hizo na kufikia uamuzi wa kuwakamata mashabiki hao mapema Jumanne na watasalia mahabusu mpaka baada ya mchezo huo siku ya Alhamisi.

 

“kupitia uchunguzi wa kina na ushirikiano wa karibu na polisi wa mji wa Paris ‘wahuni hawa wa Paris’ walikamatwa maeneo mbalimbali ikiwemo kituo cha treni na hoteli mbalimbali, pamoja na vitu vingine wamekamatwa na mask za kuzuia moshi wa mabomu ya machozi hivyo kuashiria walijipanga kwa vurugu. Watasalia mpaka mahabusu mpaka Alhamisi kwa amri ya jaji” – imeeleza taarifa ya polisi

Related Articles

Back to top button