Kwingineko

Christina Shusho: sina tofauti na Diamond  

DAR ES SALAAM: Msanii mahiri wa muziki wa Injili, Christina Shusho, amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, akieleza kuwa hana tofauti naye na kumtaja kuwa ni mtu mwema mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari, Shusho amesema kuwa hakuna tatizo lolote baina yao na kuwahimiza Watanzania kutambua umuhimu wa Diamond katika kukuza sanaa ya uimbaji.

“Diamond Platnumz ni mtu mwema, sina shida naye hata kidogo. Kama tukipata nafasi ya kufanya kazi pamoja, niko tayari. Haijalishi anakuja kwa nafasi gani au anaomba wimbo wa aina gani — sote ni wanadamu, ni watu wa Mungu, tumeumbwa na Mungu, na tukiimba pamoja naamini tutamtukuza Mungu,” amesema Shusho.

Kauli hiyo imekuja kufuatia uvumi ulioenea kwamba kuna sintofahamu kati ya wasanii hao wawili katika maandalizi ya tamasha Mtoko wa Pasaka, lakini Shusho amesisitiza kuwa hakuna mgogoro wowote uliopo baina yao.

Aidha, ameongeza kuwa wasanii wengi wa Bongo Fleva wamekuwa wakimwomba kufanya nao kazi, lakini mara nyingi ratiba zake zimekuwa zimebana, jambo linalomfanya ashindwe kutimiza maombi hayo kwa wakati.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button