Burudani

Makonda ampokea Fally Ipupa, ahidi kutoa burudani ya historia

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amempokea msanii maarufu wa muziki wa Rhumba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fally Ipupa, aliyewasili nchini kwa ajili ya kutumbuiza katika tamasha linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, Lugalo Golf jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokelewa, uwanja wa ndege wa kimataifa Fally Ipupa
amesema Watanzania wanapaswa kujiandaa kupata burudani nzuri kutoka kwake, akieleza kuwa ana matarajio ya kuwapa mashabiki wake burudani ya kipekee kupitia muziki wake.

Msanii huyo ambaye ni miongoni mwa majina makubwa katika muziki wa Rhumba na Afro-Rhumba barani Afrika, anatarajiwa kukutana na mashabiki wake wa Tanzania katika onyesho hilo litakalofanyika Lugalo Golf.

Mapokezi ya msanii huyo na Waziri Makonda yanaonesha umuhimu wa kuendelea kutumia matamasha ya muziki kama sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni na kukuza sekta ya burudani nchini.

Related Articles

Back to top button