Muziki

Kanye West avunja rekodi ya shoo Marekani

TEXAS: RAPA Kanye West ameweka rekodi ya mahudhurio makubwa ya tamasha katika historia ya muziki wa Hip-Hop nchini Marekani.

Ripoti ya Mtandao wa Hip Hop All Day, imebainisha kuwa tamasha lake lililofanyika Uwanja wa Reliant mjini Houston juzi, limehudhuriwa na mashabiki 80,210.

Hiyo, imevunja rekodi ya awali ya Kanye au Ye iliyowekwa katika Uwanja wa SoFi mwezi Aprili, mwaka huu ambapo aliuza zaidi ya tiketi 74,000 kwa kila shoo ambayo ilifanyika kwa siku mbili.

Kwenye shoo ya Houston, Ye aliwapandisha jukwaani, mwanawe North West, André Troutman, na Playboi Carti ili kutumbuiza nyimbo walizoshirikiana pamoja na nyimbo nyingine za wasanii hao.

Aidha, bosi huyo wa chapa ya Yeezy, akiwa jukwaani hapo aliwashukuru mashabiki kwa kuvunja rekodi hiyo muhimu pamoja na kumuunga mkono kwa miaka yote.

“Tumevunja rekodi. Hili ndilo tamasha kubwa zaidi la (rap) katika historia ya Marekani. Asante, H-Town. Asanteni nyote kwa kuwa nami bega kwa bega kwa miaka hii yote.”

Hata hivyo, hili si tamasha kubwa zaidi katika historia ya Kanye West. Mei, mwaka huu 2026, Ye alitumbuiza mbele ya mashabiki 118,000 jijini Istanbul, Uturuki.

Related Articles

Back to top button