BurudaniMuziki

Mwimbaji wa ‘Loliwe’ afariki dunia

MTUNZI na mwimbaji wa muziki Afro-pop wa Afrika Kusini, Bulelwa Mkutukana, maarufu Zahara amefariki dunia.

Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini, Zizi Kodwa amesema Zahara alikuwa amelazwa hospitali kutokana na kilichoripotiwa kuwa matatizo ini.

“Zahara na gitaa lake wameleta matokeo kustaabisha na ya kudumu katika muziki wa Afrika Kusini,” amesema Kodwa kupitia mtandao wa X.

Mwaka 2019 Zahra alifunguka kuhusu vita yake dhidi ya uraibu wa pombe.

Alishinda tuzo mwaka 2011 kutokana na albamu yake ya Loliwe iliyopendwa kote Afrika.

Zahra ambaye aliachia albamu tano, alishinda tuzo kadhaa za ndani na nje.

Related Articles

Back to top button