Muziki

Blue Ivy apanda jukwaani na Jay-Z, Destiny’s child yaungana tena

LOS ANGELES: BINTI wa mwanamuziki maarufu Beyoncé na rapa Jay-Z, Blue Ivy Carter, amevutia mashabiki baada ya kupanda jukwaani na baba yake katika tamasha lililowakutanisha mastaa wa muziki na kuibua hisia miongoni mwa mashabiki.

Blue Ivy, ambaye amekuwa akijitokeza katika matukio mbalimbali ya muziki akiwa pamoja na mama yake, aliendelea kuonesha kipaji chake, akivutia mashabiki waliokuwa wakifuatilia tukio hilo.

Katika tukio hilo, Blue Ivy alionekana akicheza kinanda, hatua iliyoongeza msisimko kwa mashabiki na kuonesha namna kizazi kipya cha familia hiyo kinavyoendelea kujihusisha na muziki.

Mbali na tukio hilo, mashabiki walipata nafasi ya kushuhudia muunganiko wa waimbaji wa kundi la Destiny’s Child, lililokuwa maarufu duniani kupitia nyimbo zilizotikisa chati za muziki miaka ya nyuma.

Kundi hilo, lililoundwa na Beyoncé, Kelly Rowland na Michelle Williams, lilikuwa miongoni mwa makundi ya muziki wa R&B yaliyopata mafanikio makubwa, likijizolea mashabiki kutokana na nyimbo na maonesho yake ya jukwaani.

Kuonekana kwa waimbaji hao pamoja kumeibua kumbukumbu za safari yao ya muziki na kuamsha shauku miongoni mwa mashabiki waliokuwa wakitamani kuona tena muunganiko wa kundi hilo.

Tukio hilo limeendelea kuonesha mvuto wa familia ya Jay-Z na Beyoncé katika tasnia ya burudani, huku Blue Ivy akizidi kutambulika kutokana na ushiriki wake katika matukio makubwa ya muziki akiwa na wazazi wake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button