Muziki

Harmonize Magoma Mfululu

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini Rajab Abdul ‘Harmonize’ ambaye pia ni msimamizi wa lebo ya ‘Konde Gang’ ametangaza kuachia albamu yake ya tano tarehe 25 Mei Mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Harmonize ameandika kupitia ‘Instastory’ yake kwa kuandika maandishi ya Kiingereza “Ms The Album, May 25 can’t wait. Making this album was special can’t wait to share this with you” yenye maana “Kuifanya Album hii ilikua ni jambo maalumu sana, nina shahuku kubwa kuwaletea”ameandika Harmonize.

Hii itakuwa ni Albamu ya tano kwa ‘Konde boy’ toka aanze muziki ambapo albamu ya kwanza iliitwa Afro East aliyoiachia mwaka 2020, iliyofuatiwa na Made For Us mwaka 2022, HighSchool 2021na Visit Bongo 2023.

Related Articles

Back to top button