Mashujaa: Yanga si ya kubezwa

DAR ES SALAAM: Kocha wa Mashujaa Amani Josiah amesema hawataichukulia Yanga kama timu rahisi kuelekea mchezo wao wa kesho, akisisitiza kuwa licha ya mabadiliko katika benchi la ufundi la mabingwa hao watetezi, bado ni timu kubwa yenye uwezo wa kupata matokeo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Kocha huyo amesema Mashujaa imetumia muda wa takribani siku saba kujiandaa kwa mchezo huo, ikilenga kuimarika kisaikolojia na kimbinu baada ya matokeo ya mchezo uliopita.
Amesema maandalizi hayo yameipa timu nafasi ya kutathmini mapungufu yake, kufanya marekebisho ya mbinu na kujiandaa kukabiliana na changamoto inayotarajiwa kutoka kwa Yanga.
Ameeleza kuwa ingawa kuna mazingira yanayoweza kuipa Mashujaa nafasi ya kupata matokeo, ikiwamo hali ya kisaikolojia ya mpinzani na uwezekano wa kukosekana kwa baadhi ya wachezaji, hilo halimaanishi kuwa mchezo utakuwa rahisi.
“Bado tunaizungumzia Yanga kama timu kubwa, tunaizungumzia Yanga kama mabingwa. Hatupaswi kuiona hali hii kama faida ya moja kwa moja kwetu,” amesema.
ocha huyo amekumbusha kuwa Yanga ilitwaa ubingwa msimu uliopita ikiwa chini ya kocha msaidizi, akitumia mfano huo kueleza kuwa mabadiliko ya benchi la ufundi hayamaanishi moja kwa moja kushuka kwa uwezo wa timu.
Amesema wataingia katika mchezo huo kwa umakini, wakitambua kuwa ushindi dhidi ya timu yenye hadhi ya Yanga unahitaji



