Kikapu

Fox Divas yaandika historia Afrika

PWANI: TANZANIA imeandika historia mpya katika kikapu cha wanawake baada ya timu ya Fox Divas kufuzu kwa mara ya kwanza kushiriki fainali za Mashindano ya klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake, zitakazofanyika Desemba mwaka huu jijini Cairo, Misri.

Fox Divas imejihakikishia tiketi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kuifunga timu ya KPA ya Kenya kwa jumla ya vikapu 102-97, katika michuano ya kufuzu iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani na hivyo kufanikiwa kuiondoa timu hiyo kongwe iliyoshiriki fainali za mashindano hayo mwaka jana.

Matokeo hayo yanaifanya Fox Divas kuwa miongoni mwa timu zitakazowania ubingwa wa Afrika, huku ikiungana na timu za Rwanda, REG na APR, ambazo pia zimefuzu kwa hatua hiyo.

Kufuzu kwa Fox Divas ni hatua muhimu kwa kikapu cha wanawake nchini, kwani kunatoa nafasi kwa timu hiyo kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa kubwa la ushindani wa klabu barani Afrika.

Related Articles

Back to top button