Kwingineko

Kane nafasi kubwa ya kushinda Ballon D’or

LONDON: NAHODHA wa timu ya taifa ya England, Harry Kane, anaonekana kuwa miongoni mwa vinara wanaowania kutwaa tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka 2026, katika hafla inayotarajiwa kufanyika jijini London leo Jumatatu, Oktoba 26.

Mshambuliaji huyo wa Bayern Munich, mwenye umri wa miaka 33, alifunga mabao 73 katika michezo 65 aliyocheza kwa klabu na timu ya taifa msimu uliopita, akisaidia klabu yake kutwaa mataji ya ligi na Kombe la Ujerumani.

Licha ya mafanikio hayo, Kane anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa nyota wa Barcelona, Lamine Yamal, mwenye miaka 19, ambaye anaendelea kuwania tuzo hiyo licha ya msimu wake kuathiriwa na jeraha la misuli ya paja Pamoja na Mbape wa Real Madrid.

Yamal ameeleza kujiamini kuhusu nafasi yake ya kushinda, akiamini kuwa mafanikio aliyoyapata yanamfanya astahili kutwaa tuzo hiyo, ingawa alikosa sehemu ya msimu wa klabu kutokana na jeraha.

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, pia ni miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo baada ya kufanya vizuri binafsi, akimaliza akiwa mfungaji bora wa La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Dunia, bila kutwaa mataji hayo.

Mshindi wa Ballon d’Or atapatikana kupitia kura za waandishi wa habari kutoka nchi 100 zilizo juu katika viwango vya FIFA. Kila mwandishi atachagua wachezaji 10 bora kutoka orodha ya mwisho ya wachezaji 30, huku pointi zikitegemea nafasi alizowapa.

Kwa upande wa wanawake, Alexia Putellas anaonekana kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu, huku Ewa Pajor akiwa mpinzani wake mkuu baada ya kufunga mabao 11 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Related Articles

Back to top button