Muziki
Diamond Platnumz aongoza kwa kutwaa tuzo za EAEA

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameibuka kinara katika Tuzo za EAEA Global Awards baada ya kutwaa tuzo nne.
Diamond Platnumz amenyakua tuzo za Mshindi kwa Ujumla wa Mwaka, Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka, Msanii Mwenye Mvuto Zaidi Jukwaani wa Mwaka na Video Bora ya Mwaka.
Katika orodha ya washindi, Juma Mkambala ‘Jux’, Zuchu na Rayvanny walitwaa tuzo mbili kila mmoja, huku D Voice, Baba Levo, Abigail Chams, Marioo, Mbosso na The African Princess wakifanikiwa kutwaa tuzo moja kila mmoja.
Ushindi huo unamfanya Diamond Platnumz kuwa msanii aliyefanya vizuri zaidi kwa idadi ya tuzo alizotwaa, huku matokeo hayo yakionesha ushindani katika tasnia ya muziki na burudani nchini.




