Nyumbani

Himid Mao: umoja ni nguvu ya Taifa Stars

DAR ES SALAAM: MCHEZAJI wa Taifa Stars, Himid Mao, amesema umoja, heshima na mshikamano ndani ya kikosi hicho ni miongoni mwa mambo yanayowapa nguvu kuelekea mchezo dhidi ya Guinea-Bissau.

Mao amesema wachezaji wamekuwa pamoja kwa miaka mingi, hali inayowasaidia kuelewana na kushirikiana kama familia, licha ya tofauti zao binafsi.

Amesema wanapokutana na changamoto au kuona jambo linalohitaji kurekebishwa, huzungumza pamoja ili kuboresha maandalizi na kuhakikisha wanaelekea kwenye mchezo wakiwa na uelewa mmoja.

Ameongeza kuwa wachezaji wanafahamu majukumu yao wanapopewa nafasi ya kuitumikia timu ya taifa, hivyo anaamini kila mmoja atajituma kutetea heshima ya Tanzania.

Akizungumzia mchezaji kijana Alphonce Mabula, Mao amesema licha ya umri wake kuwa mdogo, ana ukomavu na uwezo mkubwa wa kucheza, akimtaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yake.

“Mabula ni mchezaji mzuri na kijana mwenye ukomavu. Akiendelea hivyo, ana uwezo mkubwa wa kufika mbali zaidi na kuisaidia timu yetu,” amesema.

Mao amewataka mashabiki wa soka nchini kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars, akisema wachezaji watajitahidi kutumia uwezo wao kuipa Tanzania heshima na kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Related Articles

Back to top button