Mastaa

Vazi la kipekee la Rihana lawa gumzo Paris

PARIS, Ufaransa: MWANAMUZIKI na mfanyabiashara maarufu Rihanna amevuta hisia katika jiji la Paris nchini Ufaransa baada ya kuonekana katika tamasha la nguli wa muziki Céline Dion, akiwa amevalia suti nyeusi yenye muonekano wa kipekee.

Mwonekano huo wa Rihanna umeendelea kuzungumziwa katika ulimwengu wa burudani na mitindo, huku vazi lake likivuta macho ya mashabiki na wapenda mitindo waliokuwa wakifuatilia tukio hilo.

Rihanna alihudhuria tamasha hilo la Céline Dion mjini Paris akiwa katika vazi lililobeba mtindo wa kisasa na wa kifahari, na kuongeza mvuto wa muonekano wake katika tukio hilo.

Mbali na muziki wake, Rihanna amekuwa akifuatiliwa pia kwa karibu kutokana na uchaguzi wake wa mavazi, hasa anapohudhuria matukio makubwa ya burudani na mitindo.

Muonekano wake wa Paris umeendelea kuwa sehemu ya gumzo, huku mashabiki na wapenda mitindo wakijadili vazi hilo la kipekee alilolivaa wakati wa kuhudhuria tamasha hilo la mwanamuziki mwenzake Céline Dion.

Related Articles

Back to top button