Mastaa

Mahakama yampa Kim Kardashian fidia ya Sh 3000

PARIS: MWANAMITINDO Kim Kardashian amepewa na mahakama fidia yake ya Euro 1 (sawa na Sh 3,000) kutokana na uvamizi wa silaha uliomtokea mwaka 2016.

Mahakama hiyo iliwasilisha kiasi hicho kama kilivyoombwa na Kim mwenyewe aliyeliita tukio hilo la kutesa akili na la kutisha ambapo Kim alifungwa kamba na kuibiwa vito vya thamani ya zaidi ya Dola milioni 9 (Sh bilioni 23.8).

Baada ya kupokea fidia hiyo, Kim na Simone Harouche ambaye naye alikuwepo katika tukio hilo, kwa pamoja wameeleza kusikia faraja na haki kutendeka baada ya hukumu kutoka.

“Tunashukuru mfumo wa mahakama wa Ufaransa kwa kututambua kama waathiriwa wa matukio ya kutisha yaliyotokea Paris mwaka 2016. Tukio hilo liliacha majeraha makubwa ya kihisia, na athari zake bado zipo nasi,” ilieleza taarifa yao ya pamoja na kuendelea:

“Uamuzi wa leo hauhusu fidia, bali unahusu uwajibikaji na kutambuliwa. Tunashukuru mahakama na kila aliyetuunga mkono katika mchakato huu, na tunatumai sasa kusonga mbele na kuendelea kupona.”

Kim alivamiwa usiku wa kuamkia Oktoba 3 mwaka 2016 na majambazi waliovaa sare za polisi katika Hôtel de Pourtalès, Paris ambapo Kim alikuwa akiishi wakati wa hafla za Paris Fashion Week.

Aidha, katika hukumu ya kesi hiyo, watu wanane walikutwa na hatia na vifungo vyao vilianzia miaka mitano mpaka nane.

Katika mwendelezo wa fidia za waathirika, mahakama iliamuru pia mtu wa mapokezi wa hoteli hiyo kulipwa Euro 109,516. Na hoteli kwa ujumla italipwa kitita cha Euro 50,000.

Related Articles

Back to top button