Muziki

Gauni la Princess Diana lapigwa mnada kwa milioni 795 baada ya miaka 32

NEW YORK: GAUNI maarufu alilovaa Princess Diana usiku ambao mume wake, Prince Charles, alikiri hadharani kuwa alikuwa amemsaliti katika ndoa yao linakwenda tena kwenye mnada katika tukio linalotarajiwa kuvuta macho ya dunia nzima.

Gauni hilo, ambalo limepewa jina la “Revenge Dress”, linatarajiwa kuuzwa New York mwezi Desemba kwa bei inayokadiriwa kufikia kati ya dola 150,000 na 300,000 ambazo ni zaidia ya milioni 795.3 za Tanzania.

Lakini thamani ya gauni hilo si kitambaa, muundo wala bei yake pekee. Ni hadithi iliyobebwa na gauni hilo ndiyo iliyolifanya kuwa moja ya mavazi yanayokumbukwa zaidi katika historia ya familia ya kifalme ya Uingereza.

Ilikuwa mwaka 1994. Usiku mmoja jijini London, macho ya dunia yalikuwa kwa Princess Diana alipowasili kwenye chakula cha jioni cha gala akiwa amevalia gauni jeusi la kuvutia lililokuwa limeacha mabega yake wazi.

Muonekano huo ulikuwa tofauti na taswira ya kawaida ya mwanamfalme iliyotarajiwa kwake.
Kilichofanya usiku huo kuwa wa kipekee zaidi ni kwamba siku hiyo hiyo, Prince Charles alikiri katika mahojiano ya televisheni kwamba alikuwa amekuwa si mwaminifu katika ndoa yake na Diana.

Badala ya kujitenga na macho ya umma, Diana alijitokeza mbele ya kamera akiwa mwenye kujiamini. Na gauni hilo likawa ujumbe.

Tangu wakati huo, vazi hilo limeendelea kujulikana kama ‘Revenge Dress’, jina linaloashiria namna Diana alivyotumia mwonekano wake kujieleza wakati ndoa yake ikiwa katika kipindi kigumu sana.

Morgane Halimi wa Sotheby’s, kampuni inayosimamia mnada huo, alisema Diana aligeuza gauni hilo kuwa moja ya ujumbe wenye nguvu zaidi aliowahi kutoa katika maisha yake.

Kwa mujibu wa Halimi, vazi hilo lilionesha kwamba mitindo inaweza kuwa zaidi ya urembo inaweza kutumika kama kinga, silaha au vyote kwa pamoja.

Gauni hilo lilitengenezwa na mbunifu Christina Stambolian na tayari lina historia ya kusaidia shughuli za hisani.

Mwaka 1997, kabla tu ya kifo cha Diana katika ajali ya gari mjini Paris akiwa na umri wa miaka 36, gauni hilo liliuzwa kwa mnada.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button