Ligi Ya Wanawake

Clara Luvanga awashukuru wachezaji wenzake

RIYADH: MSHAMBULIAJI mahiri wa klabu ya Al Nassr Wanawake, Mtanzania Clara Luvanga amewashukuru wachezaji wenzake na maalum kocha wake, Abdulaziz Al-Alwni.

Clara ametoa shukran hizo baada ya juzi timu yake hiyo kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Saudi Super Cup kwa kuitandika Al Hilal mabao 4-1.

Katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa King Fahd mjini Taif, Clara alitupia ‘hat-trick’ na kuipa timu hiyo ubingwa huo kwa msimu wa pili mfululizo.

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, Clara aliandika ujumbe huo na kudokeza kuwa mpaka sasa amefunga mabao 17 dhidi ya Al Hilal.

“Sina mengi ya kusema zaidi ya asante kwa wachezaji wenzangu, makocha na mashabiki kwa kuwa nami. Pia, asante sana kocha Aziz. Na sijataja nina mabao 17 kwenye dabi,” aliandika Clara.

Nao Nassr kupitia ukurasa wao wa Instagram, waliweka picha ya Clara akiwa na kombe hilo na kuuliza swali kuwa msimu unaanza, tuzo ziko wapi? Wakimaanisha mchezaji huyo ni halali yake kunyakua tuzo lukuki msimu huu.

Related Articles

Back to top button