Africa

Kikosi cha Simba kimewasili Malawi tayari

LILONGWE: KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba kimewasili Lilongwe nchini Malawi tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Might Wanderers utakaochezwa Jumapili.

Kocha wa Simba, Steven Barker, amesema wako na tahadhari zote wakijua ubora wa wapinzani wao hivyo, wamejipanga huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza umakini katika kila eneo la mchezo.

Barker amesema Simba imepata muda mzuri wa kurejesha utimamu wa mwili na kujiandaa kwa mchezo huo utakaochezwa Jumapili.

“Tumepata wakati mzuri wa kurejesha utimamu wa mwili, jambo muhimu kufanya vizuri na kuvuka hatua hiyo. Tumeweka umakini katika kila eneo. Tuko tayari kwa mchezo wa Jumapili,” amesema Barker.

Kocha huyo amesema Simba inawaheshimu wapinzani wake, lakini itapambana kwa nguvu ili kupata matokeo mazuri.

“Wapinzani ni wazuri, tutacheza kwa kupambana na kuwaheshimu vizuri. Tunahitaji kuongeza umakini,” amesema.

Simba inatarajia kufanya mazoezi leo jioni jijini Lilongwe, ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya mwisho kuelekea mchezo huo.

Related Articles

Back to top button