Muziki

Patoranking atua Nairobi kabla ya kuachia albamu ya ‘WORLD BEST’

NAIROBI: Msanii maarufu wa Nigeria, Patoranking, aliwasili jijini Nairobi kwa ajili ya kukutana na wadau wa muziki na kutambulisha album yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, ‘World Best.’

Patoranking alifanya hafla maalum ya kusikiliza albumu hiyo katika eneo la Westlands, Nairobi, ambapo aliwakutanisha wasanii, wawakilishi wa kampuni za muziki, vyombo vya habari pamoja na wadau wengine wa sekta ya burudani.

Katika hafla hiyo, Patoranking aliwasilisha nyimbo zote 15 zilizokuwa kwenye album hiyo, huku miongoni mwa wageni waliokuwepo wakiwa ni Bien-Aimé Baraza na Chimano kutoka Sauti Sol pamoja na wadau mbalimbali wa muziki.

Album “World Best” ilikuwa album ya nne ya Patoranking na ilitarajiwa kuendeleza mchanganyiko wake wa Dancehall, Reggae na Afrobeats. Album hiyo ilitolewa rasmi Septemba 6, 2023.

Album hiyo pia ilikuwa na ushirikiano na wasanii mbalimbali, akiwemo Diamond Platnumz, Kizz Daniel, Beenie Man, Gyakie, Victony, Ludacris na Popcaan.

Related Articles

Back to top button