Burudani

Pipy Tida: Ukitukana kwenye dukuduku jela miezi mitatu

DAR ES SALAAM: Mtangazaji wa kipindi cha Dukuduku, Pipy Tida, ameweka wazi kuwa kuanzia sasa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayetumia lugha za matusi au kumtukana mwenzake kupitia kipindi cha Dukuduku.

Kauli hiyo imekuja baada ya Pipy Tida kuitwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, pamoja na Kamati ya Maadili, kufuatia mijadala na maudhui yanayohusishwa na matumizi ya lugha zisizofaa.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Pipy amesema kipindi cha Dukuduku kitaendelea kuwa sehemu ya mijadala, lakini washiriki wanapaswa kuzingatia heshima na taratibu zilizowekwa, badala ya kutumia matusi au lugha zinazoweza kuvunja sheria.

Amesema kuanzia sasa mtu yeyote atakayekiuka utaratibu huo atakutana na mkono wa sheria, akiwataka washiriki na watazamaji kutumia lugha yenye staha wanapotoa maoni yao.

“Ukitukana utakutana na mkono wa sheria!”
Pipy amesisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha Dukuduku inaendelea kuwa jukwaa la mijadala yenye tija, huku ikizingatia maadili, heshima na sheria za nchi.

Kauli hiyo inakuja wakati ambapo mijadala ya mitandaoni na vipindi vya burudani imekuwa ikivuta hisia za umma, huku baadhi ya washiriki wakitumia lugha kali wanapojadili masuala mbalimbali.

Pia amemshukuru Waziri kwa msamaha waliopewa kwa makosa mbalimbali ya kimtandao.

Related Articles

Back to top button