Rema atua Kenya na ndege binafsi, Lauryn Hill kushiriki Tamasha la Walker
![](https://spotileo.co.tz/wp-content/uploads/2024/09/IMG-20240926-WA0005.jpg)
NAIROBI: Nyota wa Nigeria Rema aliyeshinda tuzo nyingi za muziki ametua nchini Kenya kwa kutumia ndege binafsi, kabla ya onyesho lake katika Tamasha la Walker Town litakalofanyika Nairobi Septemba 28, mwaka huu.
Mshindi huyo wa Mavin Records atashiriki katika jukwaa moja na wakali wa akiwemo Bien-Aime, Buruklyn Boyz, Fathermoh, Tipsy Gee, Maandy Kabaya, Harry Craze na Wadagliz.
Mwingine atakayetumbuiza ni mwanamuziki na rapa wa Uingereza ArrDee.
Tamasha hilo pia limeshirikisha Ma-djs mbalimbali akiwemo DJ Grauchi, DJ Pierra Makena, DJ Protégé, DJ Sirm, DJ Kaneda, DJ Mista C na DJ PsKratch, pamoja na MCs Kwambox na Benvic.
Siku ya pili ya tamasha hilo itajumuisha mwanamuziki aliyeshinda tuzo ya Grammy mara nane Lauryn Hill, ambaye ni mwanachama mwanzilishi wa ‘The Fugees’ na anayetambulika duniani kote kwa mchango wake mkubwa katika hip-hop, R&B na muziki wa soul.
Albamu ya ‘The Fugees’ ya mwaka 1996 ya ‘The Score’ ilifafanua upya hip-hop, huku wimbo bora wa pekee wa Bi. Hill ‘The Miseducation of Lauryn Hill’ uliimarisha urithi wake kama mmoja wa wasanii mashuhuri na wa kudumu wa kizazi chake.
Watakaotumbuiza siku ya pili ya tamasha hilo ni mwimbaji wa muziki wa hip-hop nchini Kenya, Nyashinski, pamoja na Ndegz, mwimbaji na mtayarishaji wa nyimbo za Afro-pop kutoka Kenya, aliyeadhimishwa kwa nyimbo kama vile “Twende Nyumbani,” “Kuruka,” na “Balaa.” DJs kwa siku hiyo ni pamoja na CNG, Red Bone, Ite, Dream, na PsKratch ambapo Mwisho, Kwambox na Amina Rabar watakuwa MCs.