Filamu

Judith: Nipo single, nataka mwanaume mwenye hela nyingi

DAR ES SALAAM: MSANII wa filamu anayefahamika zaidi kupitia tamthilia ya Juakali, Judith Actress, amesema bado hajawa katika mahusiano yoyote ya kimapenzi na kwa sasa anaendelea na maisha yake akiwa single.

Akizungumza kuhusu maisha yake ya mapenzi, Judith amesema bado hajampata mtu anayekidhi vigezo anavyovitaka kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa kudumu.

“Bado nipo single, bado sijapata mahusiano,” amesema Judith Actress.

Msanii huyo ameweka wazi baadhi ya sifa anazozitafuta kwa mwanaume anayetarajia kuwa naye katika mahusiano, akisema anatamani kuwa na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha, anayejitunza na mwenye shughuli zake binafsi za kujiajiri.

Judith ameeleza kuwa mwanaume wa ndoto zake anapaswa kuwa na fedha nyingi, asiwe na kitambi, awe mrefu na asiwe ameajiriwa bali awe amejiajiri.

“Nataka mwanaume mwenye hela nyingi, asiwe na kitambi, mrefu na asiwe ameajiriwa,” amesema.

Kauli hiyo imezua mjadala miongoni mwa mashabiki na wadau wa burudani katika mitandao ya kijamii, ambapo baadhi wameunga mkono vigezo hivyo huku wengine wakivitazama kama matakwa ya kawaida ya mtu anayechagua mwenza anayemtamani.

Licha ya maoni tofauti yaliyojitokeza, Judith ameonekana kuwa wazi kuhusu kile anachokihitaj katika maisha yake ya kimapenzi, akisisitiza kuwa bado anasubiri kupata mtu anayelingana na matarajio yake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button