Ligi Kuu

Barker afichua kilichomshangaza Kagera

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba, Steven Barker amesema ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar haukuwa mwepesi, akifichua kuwa mfumo wa wapinzani wao wa kutumia mabeki watatu na wachezaji wa pembeni waliokuwa wakipanda mara kwa mara kushambulia uliwasababishia matatizo mwanzoni mwa mchezo.

Barker amesema Simba ililazimika kufanya marekebisho baada ya kuona Kagera ikitawala umiliki wa mpira, huku akieleza kuwa timu yake ilifanya makosa ya kupoteza mpira katika kipindi cha kwanza kabla ya kupata bao muda mfupi kabla ya mapumziko.

“Haikuwa mechi rahisi, hasa ikiwa ni mchezo wetu wa kwanza ugenini. Kagera ilinishangaza kwa uwezo wao wa kumiliki mpira lakini tulifanya marekebisho tukafanikiwa,” amesema Barker.
Kocha huyo amesema baada ya mapumziko Simba ilianza vizuri zaidi kabla ya kadi nyekundu kubadilisha mpangilio wao, lakini kuingia kwa Elie Mpanzu kulisaidia kupata bao la pili na kutoa utulivu zaidi.

“Mpanzu alipoingia, Labase alifanya vizuri na kumpa pasi nzuri, kisha Mpanzu akamzunguka kipa na kufunga. Bao hilo lilikuwa muhimu kwa sababu lilitupa nafasi ya kuongoza kwa mabao mawili,” amefafanua.

Barker ameongeza kuwa katika dakika 15 hadi 20 za mwisho, Simba ililazimika kuwa na nidhamu zaidi katika ulinzi, ikidhibiti nafasi na kuzuia Kagera kupata nafasi za kufunga.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button