Ligi KuuNyumbani

Pluijm atambia kikosi chake

KOCHA Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amesema ubora na mshikamano wa uchezaji kwenye kikosi hicho unampa matumaini ya ushindi katika mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Azam.

Azam itaikaribisha Singida Big Stars kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam Oktoba 3.

Akizungumza na Spotileo kocha huyo amesema uwezo unaooneshwa na wachezaji wa timu hiyo vinampa nguvu na kwenda Chamazi akiwa na uhakika wa kuondoka na pointi tatu.

“Azam ni timu nzuri imesajili vizuri lakini nadhani Singida ina timu bora na imara zaidi kuliko ilivyo Azam ndio maana naamini tutashinda bila kujali kwamba tutakwenda kwao,” amesema Pluijm.

Pluijm amesema maandalizi ya kikosi chake yanakwenda vizuri na wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo na mingine ya ligi.

Related Articles

Back to top button