Nyumbani

Simba, Yanga nje 10 bora CAF

CAIRO: ORODHA ya viwango vya timu za klabu Afrika imetoka na Simba na Yanga zipo nje ya 10 bora.

Simba ambayo mwaka jana ilikuwa nafasi ya tano, inashika nafasi ya 11 kwa pointi 38, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 35 ambapo mwaka jana pia ilikuwa kwenye nafasi hiyo kwa pointi 34.

Timu nyingine za Tanzania zilizochomoza ni Azam inayoshika nafasi ya 39 kwa pointi 5 na Singida Black Stars yenye pointi 2.5 katika nafasi ya 58.

Kwenye 10 bora, Mamelodi Sundowns inaongoza, ikifuatiwa na Al Ahly, Esperance de Tunis, RS Berkane, USM Alger, Zamalek, Pyramids, AS FAR, Al Hilal na CR Belouizdad.

Aidha, katika droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba itaanza hatua ya awali ikipepetana na Might Wanderers ya Malawi.

Yanga yenyewe imepangwa kukipiga na Gaborone United ya Botswana.

Na katika Kombe la Shirikisho Afrika, Singida itacheza na Al Ghalaza ya Sudan huku Azam ikianzia raundi ya pili ya awali ikisubiri mahindi baina ya Zed FC ya Misri dhidi ya ASAS Djibouti ya Djibouti.

Mechi zote za Tanzania katika raundi ya kwanza ya awali zitaanzia ugenini zikitarajia kuminyana Septemba 4 hadi 6 wakati za marudiano zikiwa Septemba 11 hadi 13, mwaka huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button