Nyumbani

Bambo aipongeza Simba, Mangungu kutwaa Kombe la Shirikisho FA

DAR ES SALAAM: Muigizaji wa vichekesho na shabiki wa klabu ya Simba, Dickson Makwaya maarufu Bambo, ameipongeza timu hiyo kwa kutwaa Kombe la Shirikisho FA.

Bambo amesema ushindi huo ni ishara ya kurejea kwa timu katika ushindani na unapaswa kuwa chachu ya mafanikio makubwa zaidi kwa mwakani.

Bambo, ambaye alionekana akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu walipotembelea banda la TSN katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), alimpongeza kiongozi huyo kwa kazi kubwa anayofanya pamoja na viongozi wenzake kuhakikisha klabu inaendelea kuimarika na kurejea kwenye mstari wa ushindi.
Bambo alisema mafanikio ya kutwaa Kombe la Shirikisho ((FA) yanapaswa kuwapa ari viongozi, benchi la ufundi na wachezaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi, huku akisisitiza kuwa mashabiki wa Simba wana matarajio makubwa ya kuona timu yao ikirejesha ubingwa wa Ligi Kuu.

Aidha, aliwataka viongozi wa Simba kujiandaa kikamilifu kuelekea msimu ujao kwa kuimarisha kikosi na kufanya maandalizi ya kutosha ili timu iweze kushindana kwa nguvu zote na hatimaye kutwaa taji la Ligi Kuu, kuwapoka wapinzani wao Yanga.

Related Articles

Back to top button