Ligi Kuu

Nduwumwe kinara wa mabao Ligi kuu

DAR ES SALAAM: PAZIA la msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu Tanzania Bara limefungwa huku mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mossi Nduwumwe, akimaliza msimu akiwa kinara baada ya kufunga mabao 17.

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum, amehitimisha msimu akiwa nafasi ya pili kwa mabao 15 na asisti tisa, huku Allan Okello wa Yanga SC akikamilisha tatu bora kwa mabao 14 na asisti Saba.

Fabrice Ngoy wa Namungo FC na Mathew Momanyi wa Pamba Jiji FC wamefunga mabao 11 kila mmoja, wakati Prince Dube wa Yanga SC na Maabad Maabad wa Coastal Union wakimaliza msimu wakiwa na mabao 10 kila mmoja.

Wachezaji waliomaliza msimu wakiwa na mabao tisa ni Mudathir Yahya, Laurindo Depu na Pacome Zouzoua wa Yanga SC, Selemani Mwalimu wa Simba SC pamoja na Paul Peter na Salehe Karabaka wa JKT Tanzania.

Idd Seleman ‘Nado’ wa Azam FC na Clatous Chama wa Simba SC wamehitimisha msimu wakiwa na mabao manane kila mmoja.

Kwa takwimu hizo, Mossi Nduwumwe ndiye anayemaliza msimu akiwa juu ya orodha ya wafungaji, huku Feisal Salum na Allan Okello wakifuatia katika nafasi ya pili na ya tatu.

Related Articles

Back to top button