Kwingineko

Bielsa:Sikuangalia kamera kwa sababu mimi siyo model

FLORIDA:KOCHA wa timu ya taifa ya Uruguay, Marcelo Bielsa, ametoa majibu makali baada ya kuulizwa kuhusu picha yake rasmi ambayo imekuwa ikizungumziwa na mashabiki katika siku za karibuni.

Bielsa alionekana kutotazama moja kwa moja kamera wakati wa upigaji picha rasmi wa mashindano, jambo ambalo lilizua maswali kutoka kwa baadhi ya mashabiki na vyombo vya habari.

Akizungumzia suala hilo, Bielsa amesema hakuona sababu ya kulielezea kwa undani.

“Sikuangalia kamera kwa sababu mimi siyo model,” amesema Bielsa.

Kocha huyo ameongeza kuwa wapiga picha walichukua picha waliyoweza kupata wakati yeye akiwa ameelekeza macho kwao, na hakuona tatizo lolote katika hilo.

“Sina haja ya kutoa maelezo yoyote. Walinipiga picha jinsi walivyonipiga. Nilikuwa nawaangalia wapiga picha na hiyo ndiyo picha waliyoipata kutoka kwangu,” amesema Bielsa.

Akiendelea kuelezea msimamo wake, amesema wakati mwingine watu hujaribu kutafuta maana kubwa kwenye mambo madogo yasiyohitaji maelezo.

“Kuna wakati kila kitu kinahitaji maelezo. Mtu akivaa miwani anaulizwa kwa nini amevaa miwani, akiangalia mbele anaulizwa kwa nini ameangalia mbele, akiangalia chini anaulizwa kwa nini ameangalia chini,” amesema Bielsa.

“Hatuna wajibu wa kujiendesha kama model ili kuheshimu madai ambayo hayana msingi.”

Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimsifu Bielsa kwa uhalisia wake na wengine wakifurahia majibu yake ya moja kwa moja ambayo yamekuwa sehemu ya utambulisho wake kwa miaka mingi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button