Nyumbani

Ahmed: Tunataka kushinda michezo yote

DAR ES SALAAM:SIMBA imesema inaendelea kuweka lengo la kushinda michezo yote iliyosalia katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikisisitiza kuwa kila mchezo uliobaki ni muhimu katika mbio za ubingwa.

Kauli hiyo inakuja kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa kesho kutwa.

Akizungumza kuhusu mchezo huo, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema licha ya tofauti ya alama kati yao na wapinzani Yanga, hawachukulii mchezo ulioko mbele yao kiurahisi.

Amesema Simba ipo nyuma kwa alama tano dhidi ya vinara, lakini bado jukumu lao ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo ili kuweka presha katika mbio za ubingwa.

“Tuna mchezo dhidi ya Tanzania Prisons na ukiangalia ni mchezo ambao unaweza kuonekana rahisi, lakini ni mgumu. Wapo katika hali mbaya ya matokeo, na timu kama hizo huwa hatari zaidi,” amesema Ahmed Ally.

Ameongeza kuwa kucheza na timu inayopambana isishuke daraja michezo ya aina hiyo mara nyingi huwa na changamoto kubwa kwa sababu huingia uwanjani kwa kujituma zaidi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button