Mudathir, Dube wampasua kichwa kocha Azam FC.
DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amekiri ubora wa safu ya ushambuliaji wa Yanga na kuahidi kuwa makini kutowapa nafasi ya kufanya mashambulizi.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga inaongozwa na Prince Dube, Jean Baleke, Kennedy Musonda, Clement Mzize, Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki, Clatous Chama na Mudathir Yahya.
Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga, utakaochezwa uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar es Salaam, Taoussi amesema ana matumaini ya kupata matokeo mazuri endapo wachezaji wake watatumia nafasi za wazi watakazozitengeneza.
“Yanga ni timu kubwa na wana kocha mzoefu. lengo la timu yetu ni kucheza vizuri na kutafuta ushindi. Tunajua ni wazuri kwenye kushambulia, tumefanyia kazi ubora huo na mapungufu yao kuyatumia kutafuta ushindi,” amesema.
Taoussi amesema watakuwa makini kwa kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao na kutumia nafasi watakazotengeneza kutafuta matokeo chanya dhidi ya Yanga.