Muziki

Vanillah awaonya wachambuzi

....hataki maoni kwenye wimbo wake mpya

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Fanuel Peter ‘Vanillah’ amesema hataki kupokea ushauri wala maoni kutoka kwa wachambuzi wa muziki kuhusu kazi yake mpya anayotarajia kuiachia hivi karibuni.

Kupitia ujumbe wake aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, msanii huyo alieleza kuwa kuna mambo mengi yamejitokeza nyuma ya pazia ambayo watu hawafahamu, lakini mara nyingi wachambuzi huanza kutoa maoni punde tu wimbo unapotoka bila kujua undani wake.

Vanillah ameandika: “Wimbo ninaotaka kuutoa sasa hivi sitaki maoni yoyote ya wachambuzi, kuna vitu vimetokea hapa kati nataka nimalize kuviongelea humo.”

Mashabiki na wadau wa muziki, baadhi wakimuunga mkono kwa kutaka kutoa ujumbe wake bila kuingiliwa, huku wengine wakiamini kuwa uchambuzi ni sehemu muhimu ya kukuza muziki na kuwapa wasanii mrejesho.

Hatua hiyo ya Vanillah inaonekana kuashiria kuwa wimbo wake mpya utakuwa na ujumbe mzito unaogusa masuala binafsi au yaliyojitokeza hivi karibuni katika maisha yake ya kisanii.

Related Articles

Back to top button