Muziki
Rihanna aikimbia nyumba yake baada ya shambulio la risasi

LOS ANGELES: MWANAMUZIKI maarufu duniani Rihanna amelazimika kuondoka katika jumba lake la kifahari jijini Los Angeles baada ya mtu mwenye silaha kufyatua risasi kadhaa katika eneo la makazi hayo.
Kwa mujibu wa polisi wa Los Angeles, mshukiwa aliyetambuliwa kama Ivanna Lisette Ortiz alifika kwenye nyumba hiyo akiwa na bunduki aina ya semi-automatic na kufyatua takribani risasi 10.
Ingawa hakukuwa na mtu aliyejeruhiwa, Ortiz amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya jaribio la mauaji.
Baada ya hali hiyo Rihanna aliamua kuhama eneo hilo kwa muda ili kutuliza akili yake baada ya hofu ya tukio hilo.




